BANDA MEDIA BLOG

No title

Matheo Anthony (kushto) akipongezwa na beki wa timu hiyo Pato Ngonyani (kulia) baada ya kufunga goli lake la kwanza Yanga
Matheo Anthony (kushto) akipongezwa na beki wa timu hiyo Pato Ngonyani (kulia) baada ya kufunga goli lake la kwanza Yanga
Mshambuliaji wa Yanga Matheo Anthony ajana aliandika rekodi mpya kwenye klabu hiyo baada ya kufunga goli lake la kwanza kwenye klabu hiyo kwenye mechi za mashindano.
Matheo amesema alimeshafunga magoli kadhaa akiwa na Yanga lakini magoli hayo aliyafunga kwenye mechi za kirafiki na si mashindano rasmi.
“Nimefurahi sana kufunga goli kwenye mchezo wa leo (jana) ni goli langu la kwanza kwenye mechi za mashindano. Nimeshafunga magoli kadhaa lakini magoli hayo yalikuwa kwenye mechi za kirafiki”, alisema Matheo.
Matheo alifunga goli lake dakika ya 51 ambalo lilikuwa ni goli la tatu kwenye mchezo huo na kuipa Yanga ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Friends Rangers kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup na kufuzu hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG