Hazard alifungua milango ya mabao kwa Chelsea baada ya kufunga goli zuri kabisa la kuchungulia kabla ya beki wa kushoto wa timu hiyo Marcos Alonso kufunga la pili kwa kumpiga tobo kipa wa Everton Maarten Stekelenburg
Diego Costa alishindilia msumari wa tatu baada ya kupiga shuti kali kufuatia kona iliyochongwa na Pedro kabla ya kwenda mapumziko.
Pedro alifunga bao la nne baada ya kipa kuutema mpira kufuatia shuti kali lililopigwa na Eden Hazard na kumfikia hatimaye kuukwamisha kiulaini.
Everton walitumia muda mwingi kucheza katika eneo lao na kushindwa kupiga hata shuti moja lililolenga langono mwa Chelsea katika muda wote wa dakika tisini huku Chelsea wakiwashambulia mithili ya nyuki waliotibuliwa.
Dondoo muhimu
- Chelsea wameshinda michezo mitano kati ya sita iliyopita kwenye Premier League msimu huu, mingi zaidi kuliko waliyoshinda msimu wote wa mwaka 2015/15.
- Kulekea bao la pili la Eden Hazard zilipigwa pasi 23 kabla ya goli hilo, pasi nyingi zaidi kuliko zote msimu huu.
- Kwa mara ya kwanza Everton wameruhusu mabao matano au zaidi kwenye Premier League tangu walivyofungwa mabao sita na Chelsea August 2014.
- Chelsea wameweza kuzuia wapinzani wao kutopiga hata shuti moja langoni mwao kwenye kipindi cha kwanza kwa mara ya kwanza kwenye Premier League tangu Januari 2013 walipocheza na Reading.
- Eden Hazard kwa mara ya kwanza tangu Februari 2014 ameweza kufunga mabao mawili au zaidi kwenye Premier League katika Dimba la Stamford Bridge.
- Diego Costa amefunga mabao mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote kwenye Premier League msimu hii (magoli 9, pasi za mabao 3).
Tags
MICHEZO KIMATAIFA