Dk. Siafu ameyasema hayo jijini Dodoma
wakati taasisi hiyo ikishiriki kwenye maonyesho ya wiki ya wabunifu MAKISATU yanaendelea
katika uwanja wajamhuri jijini humo
Amesema serikali imeanzisha programu hiyo inayofadhiliwa na Shirika la watoto Duniani (UNICEF) kwa lengo la kuwasaidia vijiana kujikwamu kiuchumi
na kuwaondoa katika unyonge wa umasikini
Amesema iposa ni mpango maalum ambao
unachukua vijana ambao hawakuwahi kusoma na wale waliosoma shule za msingi na
za sekondari ambapo wana vipaji vya ubunifu na kupelekwa shule za ufundi kupitia
taasisi hiyo ya elimu ya watu wazima ambayo maombi ya kujiunga ni bure kupitia ofisi za Elimu ya watu wazima zilizopo kila mkoa
Wabunifu Musa Chengula na Frank Mselu wakimuelezea jambo kuhusu mfumo wa kuongoza magali walioubuni kwa kutumia Roboti (KUSHOTO NI MTEJA)
“wawalete sisi kwa sasa tunafundisha
kisomo na ufundi wa awali ambavyo vyote
vianamsaidia mwanafunzi ambaye hakuwahi kusoma kabisa kuingia katika mfumo
kwani kutokana na ubunifu lazima afike mbali
“hivi sasa tupo katika maonyesho haya
na vijana hawa mnaowaona walikuja kujiunga tena kwa kuchagua fani waipendayo
kama vile Umeme, uselemala, Tehama na wameweza kubuni vifaa mbalimbali kama
vile Robotics, Rade security, Mathematcs Game, Motion Detetor, Securty, Trafic
Light na Enqubetor”, alisema
Naye Afsa Elimu na Mratibu wa IPOSA kasulu T/c Kigoma Felician Ferdinand alisema tayari wamesha wasajili wanafunzi elfu 12 katika mikoa 9 ya Tanzania bara ambapo mwezi ujao wataifikia mikoa mingine 6 na kuwa na jumala ya miakoa 15 hivyo kuwataka vijana waliokosa kusoma kupata nafasi ya kusoma tena
"programu hii ya IPOSA iliyodhaminiwa na shirika la watoto Duniani UNICEF ni mpango utakaodumu kwa miaka 8 ukitarajiwa kuwanufaisha vijana wengi zaidi ambao walikuwa wamekata tamaa kutokana na kukosa elimu",
Daud Yudas