RC CHALAMILA APONGEZA UKAMATAJI WA MADAWA YA KULEVYA
*Atoa pongezi nyingi kwa Rais Dkt Samia kwa uteuzi wa Kamishna
Aretas Lymo
*Akiri DSM kuwa ndio lango la
kuingizia na kuzisafirisha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe. Albert Chalamila ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za
Kulevya Nchini DCEA ambapo imefanikiwa kukamata kg 3,182 za dawa za kulevya
aina ya Heroin na Methamphetamine katika oparesheni maalum iliyofanyika Jijini
Dsm
RC Chalamila amesema pongezi
nyingi zimwendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwa kufanya uteuzi Mzuri wa Kamishna Jenerali Aretas Lyimo wa Mamlaka
hiyo ambaye kwa kushirikiana na timu yake kuonyesha uzalendo na weledi Mkubwa
Kudhibiti biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya Nchini
Aidha, Mkuu wa Mkoa amekiri kuwa DSM ndio lango la kuingizia na
kuzisafirisha dawa hizo haramu ambapo husambaa nchi nzima hivyo ametaka vijiwe
vyote vinavyofanya biashara hii harumu kukomeshwa Mara moja
Wakati huo huo RC Chalamila
amesema kikosi kazi tayari kimeundwa ili kupambana na biashara hiyo haramu
sambamba na kuwakamata wakwepa Kodi na vibaka
Kwa upande wake Kamishna
Jenerali wa DCEA Aretas Lymo amesema oparesheni hii ni endelevu na kila
atakayejihusisha na biashara hii haramu atakamatwa na Sheria itachukua mkondo
wake
Hata hivyo, Kamanda wa Kanda
maalum ya kipolisi Dsm Afande Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi
litahakikisha linakata mashina yote na kuyamaliza madawa hayo haramu kabisa
