(Katikati) ni hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kushoto Mama Fatma Karume na kulia ni Fatma Karume
............
Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, amefariki dunia.
Taarifa za kifo chake zimefika wakati akiwa nyumbani kwa Mmoja ya watoto wake huko Zanzibar.
Mama Fatma Karume alikuwa mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar, ambaye aliongoza Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Mama Fatma Karume anafariki akiwa na umri wa miaka 97.
