.................
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa Viongozi 114, wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Septemba 29, 2026, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu kati ya Viongozi hao 51 wameteuliwa, huku 63 wakihamishwa katika maeneo mbalimbali.
Katika nafasi za Wakuu wa Wilaya, watu 22 wameteuliwa na 26 wamehamishwa, huku kwa Makatibu Tawala wa Wilaya 12 wakiteuliwa na wanne wakihamishwa.
Kwa upande wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, 17 wameteuliwa, huku 33 wakihamishwa kwenda katika Halmashauri mbalimbali Nchini ambapo uteuzi na uhamisho huo unaanza mara moja.
#BANDAMEDIAUPDATES

Tags
UTEUZI