BANDA MEDIA BLOG

DOUMBIA AANZA KWA KISHINDO, AFUNGA MAWILI DHIDI YA 15 DE AGOSTO

 Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameanza vizuri kampeni ya kutinga hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa 15 de Agosto mabao 6-1 katika mchezo uliopigwa Oktoba 21, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Huku Ibrahim Doumbia akitakata kwa kuanza kufunga magali 2 katika mchezo huo. 

Katika mchezo huo, Nathaniel Chilambo alianza kuifungia Simba dakika ya 42, kabla ya Elie Mpanzu kuongeza bao la pili dakika ya 55. Ibrahim Doumbia alifunga bao la tatu dakika ya 64 na kuongeza la nne dakika ya 81, huku Keletso Makgalwa akitikisa nyavu dakika ya 71 na Anicet Oura akafunga bao la sita dakika ya 82.

Matokeo hayo yameiweka Simba katika nafasi nzuri ya kusonga mbele na kutinga hatua ya makundi, ingawa bado inahitaji kuthibitisha nafasi hiyo katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 25, 2026, jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Doumbia ameweka alama muhimu katika safari yake ya Simba kwa kufunga mabao yake ya kwanza tangu asajiliwe na klabu hiyo. Mshambuliaji huyo amefunga mabao mawili katika mchezo huo, akichangia ushindi mnono wa timu yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG