Balozi wa Israel Nchini Mhe. Yahel
Vilan akiongea jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na
Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake
katika Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 4, 2017
Dodoma.
Mwambata Jeshi wa Israel Barani
Afrika Bw. Aviezer Segal akionesha michoro ya muundo wa Ofisi yake
wakati wa ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Idara
ya Maafa ili kuangalia eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Kituo
cha Kitaifa na Kimataifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura,
Dodoma.
Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu
wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi akionesha muundo wa
Idara hiyo wakati wa ziara ya ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan
katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Aprili 4, 2017.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza mwenye miwani)
akifuatilia mada ya muundo wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati
wa Ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan Dodoma.
Wakala wa Maendeleo wa Kimataifa
wa MASHAV Bw. Yuval Fuchs akitoa hoja wakati wa Ziara ya Balozi wa
Israel Mhe. Yahel Vilan kwa Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
Dodoma.
Waziri Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na baadhi wa
wageni walioambatana na Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan alipotembelea
Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 4, 2017 Dodoma.
Mkurugenzi wa Idaya ya Uratibu wa
Maafa Ofisi ya Waziri Brig. Jenerali, Mbazi Msuya (wa kwanza kushoto)
akimuonesha Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan ramani ya eneo
lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa na Kimataifa cha
Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati waliokaa) akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya Watendaji wa Serikali
walioshiriki katika ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan mara
baada ya kumpokea Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)
Tags
OWM- MAAFA